Suala la utata wa mkataba kati ya
klabu ya Simba na kiungo wake Ramadhani Singano linaonekana kuwa gumu.
Kwani pamoja na Kamati ya Sheria, Maadili
na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kukaa
leo, lakini bado jibu halijapatikana!
Sasa suala hilo litawakutanisha tena wiki
ijayo kwa ajili ya kujua kipi hasa ni sahihi na kipi ni kosa.
Mwenyekiti wa Sputanza, Mussa Kisoki
amesema kuwa mambo yamekwenda vizuri lakini watakutana tena wiki ijayo.
“Tumekaa kweli, lakini bado naweza
kusema kuna mambo kadhaa ya kujadili na mwenyekiti wa kamati amesema tukutane
wiki ijayo,” alisema.
Kisoki alikataa kuelezea walipofikia
na kusisitiza ni kazi ya mwenyekiti wa kamati huyo ambaye ilikuwa mbinde
kumpata.
Tofauti kati ya Singano maarufu kama
Messi na Simba ilianza baada ya kiungo huyo kusema mkataba wake unaisha mwaka
huu na ulikuwa wa miaka miwili.
Lakini Simba walisisitiza, mkataba
huo unaisha mwakani kwa kuwa ulikuwa wa miaka mitatu.
Hata hivyo, TFF ilikubali
kusuluhisha, lakini pande hizo mbili huku Messi akisimamiwa na Sputanza,
likavurugika zaidi na Simba ikasisitiza lipelekwe kwenye kamati ili kupata
mwafaka.
Kushindwa kupatikana kwa mwafaka leo,
inaonyesha kuna jambo ambalo linaongeza ugumu na vema likajulikana.
0 COMMENTS:
Post a Comment