June 27, 2015

 Mashabiki wa Yanga sasa roho kwatu baada ya leo kutambulishwa mshambuliaji wao mpya, Donald Ngoma.

Mashabiki hao wamemuona Ngoma raia wa Zimbabwe baada ya kuwasili na kupelekwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambako Yanga ilikuwa inaivaa SC Villa ya Uganda katika mechi yao ya kirafiki.
Ngoma alitua uwanjani hapo akifuatana na baadhi ya viongozi na wanachama wa Yanga.

Pia kiungo mkabaji mwenye uwezo wa kucheza beki, Joseph Tetteh Zutah raia wa Ghana ni kati ya waliotua leo kwa ajili ya kumalizana na Yanga.

Ngoma aliwasalimia mashabiki wa Yanga ambao walishangilia kwa nguvu huku wakitumia muda huo kuwabeza wenzao wa Simba walionekana kuwa kimya.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic