June 1, 2015

AMROUCHE (KULIA) AKIWA NA MSAIDIZI WAKE.

Na Saleh Ally
Kocha maarufu raia wa Ubelgiji, Adel Amrouche amesema kamwe hajawahi kuwania kuinoa Simba.


Akizungumza na SALEHJEMBE kutoka Brussels nchini Ubelgiji, Amrouche mwenye asili ya Algeria amesema hajawahi kuwania kuinoa Simba.

"Nimesikia kutoka kwa rafiki yangu kwamba nawania kuifundisha Simba, si kweli.
....AKIWA NA MOSES ODHIAMBO.
"Inawezekana wao wangependa iwe hivyo, ila ndoto yangu ni kufanya vizuri katika michuano ya Afrika nikiwa na timu ya taifa.

"Ingekuwa timu ya taifa ya Tanzania, sawa lakini klabu, niwe mkweli si ndoto yangu," alisema Kocha huyo bora wa Ukanda wa Afrika Mashariki na KAti.

Amrouche alibeba tuzo ya kocha bora Afrika Mashariki na Kati baada ya kuiwezesha Kenya iliyokuwa na kikosi dhaifu, kubeba ubingwa wa Cecafa.

Pia Amrouche amekuwa mmoja wa makocha waliokifanya kikosi cha timu ya taifa ya Burundi kuwa moto.

Kabla ya kuifundisha Burundi, aliwahi kuwa kocha wa DC Motema Pembe ya DR Congo na kuiwezesha kubeba mataji lukuki.

Hivi karibuni, vyombo vya habari viliripoti kwamba Amrouche alikuwa kati ya makocha wanaowania kuinoa Simba.

Hata hivyo, uongozi wa Simba, bado haujatangaza kocha yupi ambaye unapambana ili kumpata baada ya zaidi ya makocha watano kuomba nafasi ya kuinoa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic