Uongozi wa Yanga, umemkabidhi
mshambuliaji wake mpya, Malimi Busungu jezi namba 16.
Busungu amekabidhiwa jezi hiyo leo
wakayi akitambulishwa mbele ya waandishi wa habari.
Straika huyo amejiunga na Yanga
akitokea Mgambo JKT ya Tanga.
Awali, Busungu alikuwa akiwaniwa na
Simba, lakini mwisho Yanga ilifanikiwa kumnasa.
Busungu amesema anaamini Yanga ni
sehemu sahihi na ana matumaini makubwa ya kufanya vizuri.
0 COMMENTS:
Post a Comment