June 12, 2015


STERLING:
Man City imekuwa ya kwanza kuweka wazi kwamba inamtaka kiungo wa Liverpool, Raheem Sterling kwa pauni milioni 25 na itaongeza juu yake pauni milioni 5 zaidi. Lakini Liverpool imegoma na kusisitiza inataka ‘dabo’.



Pamoja na Man City, Chelsea, Arsenal na Real Madrid nazo zimeonyesha nia za kumnasa Mwingereza huyo mwenye asili ya Jamaica.

Pogba:
Wakati ilionekana kama atatua Madrid, wapinzani wao Barcelona wameeleza wazi kutaka kumnasa Paul Pogba.

Tayari Juventus imeishaweka dau na kusema inataka pauni milioni 55.

Madrid imeendelea kusisitiza inamtaka kipa David De gea kwa pauni milioni 30 na Chelsea nayo imeonyesha nia ya wazi kwa mshambuliaji Radamel Falcao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic