Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula kesho
jumamosi atafunga rasmi mashindano ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka
13.
Sherehe ya kufunga mashindano hayo itafanyika katika
uwanja wa CCM Kirumba kuanzia majira ya saa9 kamili alasiri .
Kwa takribani wiki moja sasa mashindano hayo yamekuea
yakiendelea jijini Mwanza katika viwanja vya Alliance na CCM Kirumba.
Lengo la mashindano haya ni kuibua vipaji kwa ajili ya
kupata timu ya Taifa ya awali itakayojiandaa na fainali za vijana Afrika wenye
umri chini ya miaka 17 mwaka 2019 fainali zitafakazonyika nchini Tanzania.
Katika kutambua na kujiunga na watanzania wenzetu
wenye ulemavu wa ngozi (Albino) siku hiyo ya tareje 13/06/2015, TFF itajiunga
na familia ya walemavu wa ngozi katika kuadhimisha siku yao kimataifa na
kuonyesha bango maalum leney kuelimisha umma juu ya ubaya wa uovu wa kuwaumiza
na kuwaua wenzetu wenye ulemavu wa ngozi.








0 COMMENTS:
Post a Comment