Na
Saleh Ally
MABINGWA
wa soka Tanzania, Yanga wamewasilisha barua kwa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) ambao ni wenyeji wa michuano ya Kombe la Kagame kwamba wanapinga kabisa
wapinzani wao wakubwa Simba, kushiriki.
Michuano
ya Kagame imepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam, taarifa zinaeleza kuanzia
Julai 11.
Baraza
la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cefaca), liliamua Simba washiriki
kama waalikwa ili kuamsha hamasa zaidi ya mashabiki kutokana na ukubwa wa kikosi
cha Simba.
Simba ndiyo mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo hivyo ndivyo vigezo viwili walivyovitumia Cecafa kuialika Simba.
Yanga
wameona hapana, wanadai kwamba wao ndiyo wenye haki, hawakubaliani na hilo.
Hapo kuna jambo ambalo hawajaliweka wazi ingawa linaeleweka, kwamba Yanga wana
hofu ya Simba.
Wanapaswa
kuwa na hofu, lakini ingekuwa vizuri wasionyeshe uoga wa aina hiyo. Wanajua
wakikutana na Simba, basi wako matatizoni. Huenda ingekuwa vizuri wajipime kwa
mara nyingine.
Kwa
upande wa Cecafa tunajua, pamoja na kutumia vigezo viwili kuwa Simba ni
mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo, timu itayosaidia kuchangamsha michuano
hiyo. Lakini ukweli ni kwamba wanataka mapato zaidi na wanajua kama ilivyo kwa
Yanga, Simba nayo ina watu wake.
Wanachoangalia
Cecafa ni kuchangamka kwa mashindano lakini ukweli hasa ni hilo la mapato. Sasa
Yanga hawataki!
Kukataa
kwa Yanga, kunaweza kukawavuruga Simba na kuona kama wananyimwa haki ya
kushiriki kutokana na hofu ya Yanga kwao. Mimi ninaona ikiwezekana, Simba
wanapaswa kuwashukuru wapinzani wao hao.
Wanapaswa
kuwashukuru kwa kuwa kikosi cha Simba hakihitaji mashindano kama ya Kagame
katika kipindi hiki. Badala yake wanahitaji kambi ya pre season ya kutosha tena
iliyokamilika kweli.
Simba
inahitaji kambi tulivu, inahitaji kwenda kujichimbia ikiwezekana kwa ajili ya
kuunda kikosi upya. Kutengeneza timu ikiwa na baadhi ya wachezaji wapya na
kocha mpya.
Kocha
mpya wa Simba anapaswa kukiona kikosi chake, kufanya mazoezi ya kutosha na kama
ni mechi, zitafuata baada ya kikosi kuwa kimeiva kwa maana ya ‘fitness’.
Mara
nyingi timu nyingi za Tanzania zimekuwa zikiingia katika janga la majeraha
kutokana na wakati mbaya kama huo wa michuano ya Kagame. Wakati inakuja
kufanyika nchini, baadhi ya timu za nchi kama Rwanda, Kenya wanakuwa ndiyo
wanatoka kwenye ligi, maana yake wako fiti.
Wachezaji
wa timu za Tanzania, wengi wanakuwa si fiti kwa vile ligi imeisha kitambo na
wanapata muda mchache wa kufanya mazoezi magumu na ya kutosha ili kujiweka sawa.
Kawaida
angalau wiki nne hadi sita, wachezaji wanapaswa kufanya mazoezi magumu. Baada
ya hapo taratibu wanapunguza ugumu wa mazoezi na kuchezea mpira zaidi. Ndiyo
kipindi ambacho angalau mechi za kirafiki zinaingia.
Ukiangalia
Simba itakuwa na muda kiasi gani wa kujiandaa. Kipindi cha muda upi wa kutosha
hadi kocha mpya awe amekiona kikosi chake na kuanza kukipanga kwa ajili ya
michuano, tena ya kimataifa.
Simba
inaweza kushindwa kuonyesha cheche zake na kocha akaonekana hana lolote, kumbe
tatizo likawa ni haraka ya kushiriki michuano hiyo.
Lakini
kwa kuwa wachezaji hawako fiti, Simba inaweza kuingia katika kusababisha baadhi
ya wachezaji wake kuumia na wakati mwingine wakawa ‘vimeo’ msimu wote na
kuifanya iwakose kwa kushindwa kuwatumia kwa asilimia mia kutokana na kuwa majeruhi.
Kuna
kila sababu ya kujipima mara mbili kwa Simba kabla ya kuingia katika michuano
hiyo. Huenda kutaka mashabiki waione timu au kupata fedha kidogo linaweza kuwa
lengo namna moja.
Bado
iko haja ya kuangalia kama lengo hilo lina faida na hasara zake ni zipi hapo
baadaye. Siwezi kuizuia Simba kuingia na kushiriki, lakini uongizi utafakari
mara mbili katika hili. Kwani furaha ya wiki mbili kwa mashabiki, bado haiwezi
kulingana na ile ya msimu mzima kama timi itaandaliwa vizuri kwa kufuata
misingi sahihi.
Bado
uongozi wa Simba unaweza kuwa unatamani kuitumia michuano hii kujiingizia
kipato. Lakini lazima iangalie hasara inayoweza kupata kwa msimu mzima.
Siwezi
kuwa rais wa klabu hiyo, lakini ningeipata nafasi hiyo angalau kwa dakika tano
tu, basi uamuzi wa kwanza ulikuwa ni kutamka hivi; “Simba haitashiriki michuano
ya Kagame”.







pre-season matches ok hawanabudi simba kutafuta nakucheza ili kuwaweka sawa kwasababu watakuwa na wachezaji pamoja na kocha mpya.kwa hili lawachezaji kuumia kuwa majeruhi kama watashiriki kagame hapana,mchezaji anaweza kuumia hata mazoezini.simba wakipata washiriki.
ReplyDelete