June 26, 2015

 
MKUDE AKIWA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM TAYARI KWA SAFARI YA AFRIKA KUSINI.
Kiungo wa Simba, Jonas Mkude amesema atapambana kadiri ya uwezo wake ili kushinda majaribio.


Mkude ameondoka jana nchini kwenda Afrika Kusini ambako atafanya majaribio katika klabu ya Bidvets.

Klabu hiyo maarufu kama Wits imetoa nafasi kwa Mkude ambaye amepewa baraka na Simba.

“Najua kutakuwa na ushindani, itakuwa ni timu ambayo inataka viwango vya juu. Lakini nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu.

“Ninajiamini lakini kuna vitu vingi vya kujifunza wakati ninapambana,” alisema Mkude.


Mkude anatarajia kuanza majaribio leo au kesho jijini Johannesburg yalipo makao makuu ya klabu hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic