Taifa Stars inatarajia kuondoka kesho
jioni ijumaa kuelekea nchini Misri kwa shirika la ndege la Ethiopia majira ya
saa 5 usiku na kufika Cairo majira ya saa 8 usiku, kisha kuunganisha safari ya
kuelekea jijini Alexandria ambapo timu mchezo huo utakapofanyika.
Mchezo kati ya Misri dhidi ya Tanzania
utachezwa katika Uwanja wa Borg El Arab kuanzia majira ya saa 1 usiku kwa saaa
za huku, sawa na saa 2 kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Waamuzi wa mchezo huo wanatokea nchini
Ethiopia ambapo ni Bamlak Tessema Weyesa (mwamuzi wa kati), Kinfe Yilma
(mwamuzi msaidizi wa kwanza), na Wolday Hailerague (mwamuzi msaidizi wa pili).
0 COMMENTS:
Post a Comment