MESSI AKIINGIA TFF WAKATI WA USULUHISHI ULIOFANYIKA SIKU CHACHE ZILIZOPITA... |
Licha ya Ramadhani Singano ‘Messi’
kuanza ‘kulainika’ na kuwataka Simba wakae na kumaliza sakata lao, uongozi wa
klabu hiyo unaona itakuwa vema suala lake na kiungo wao likatolewa msimamo na
vyombo husika vya mpira au vile vya dola.
Habari za kutoka ndani katika kikao cha
kamati ya utendaji cha Simba kilichokutana jana, zimeeleza uongozi umeona hilo
litakuwa sahihi kabla ya mengine kufuatia.
“Wamekutana wajumbe na kuzungumza
kuhusiana na hilo. Unajua walichoona pale ni kuchafuliwa jina na kuna watu
wamekuwa wakisema uongozi umegushi mkataba.
“Uongozi wa sasa haikuingia mkataba na
Messi, kama ungekuwa umegushi, ule mkataba mama uko TFF, basi nayo imegushi.
“Lakini inaonekana katika mkataba wa
Messi ambao amesema unaisha 2015, ndiyo wenye matatizo mengi. Kumkubalia leo
kwamba yameisha, ni kuionyesha jamii kwamba Simba ina tatizo.
“Makubaliano ni kwamba lazima lazima
ukweli uwekwe hadharani. Kama kuna kugushi, nani alifanya hivyo na ikiwezekana
hatua za kisheria zichukuliwe.
“Viongozi kwa pamoja wamekubaliana hilo
litekelezwe ili kufuta kashfa inayoonekana kusukumiziwa kwa Simba wakati haipo,”
kilieleza chanzo.
Katika kikao hicho cha kamati ya
utendaji, Simba ilijadili mambo mbalimbali yakiwemo ya usajili, mwenendo wa
msimu mpya likiwemo hilo la Messi.
Suala hilo limekuwa likiipekeka Simba
puta hasa baada ya kiungo huyo kusema mkataba wake unaisha mwaka 2015 huku
Simba ikisisitiza unaisha 2016.
0 COMMENTS:
Post a Comment