Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa
na bia ya Kilimanjaro Premier Lager, kesho siku ya Ijumaa jioni inatarajiwa
kuondoka Addis Ababa Ethiopia kuelekea nchini Misri tayari kwa mchezo wa siku
ya jumapili.
Stars ambayo imeweka kambi ya mazoezi takribani kwa
wiki moja sasa jijini Addis Ababa leo imeendelea na raiba yake ya mazoezi
katika uwanja wa Taifa, amabpo leo imefanya mazoezi yake asububuhi tu.
Kocha mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij amesema,
anashukuru maendeleo ya kambi ni mazuri timu yake inafanya mazoezi katika
viwanja viwili vizuri vilivyopo Addis Ababa, uwanja wa Taifa na uwanja wa
Benki ya Biashara ya Ethiopia.
Nooij amesema amekuwa akiwafundisha wachezaji wake
kucheza mpira wa kasi na pasi za haraka haraka, jambo ambalo wachezaji
wameonyesha kufuata vizuri maelekezo yake na kusema wanamuelewa vizuri.
Akiongelea mchezo dhidi ya Misri siku ya jumapili,
Nooij amesema timu inakwenda kupambana kusaka matokeo mazuri katika mchezo,
nafahamu tunaenda cheza ugenini, nimewaelekeza vijana wangu wanaocheza nafasi
ya ushambuliaji kutumia vizuri nafasi tutakazozipata katika mchezo huo.
Aidha kocha Nooij amesema katika mpira hakuna
kinachoshindikana, kambi ya wiki moja Addis Ababa imewasaidia wachezaji kukaa
pamoja na kushika maelekezo yake vizuri, hivyo anaamini timu yake itafanya
vizuri katika mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON.
Katika kikosi cha wachezaji wa 22 waliopo kambini
jijini Addis Ababa hakuna mchezaji majeruhi, wachezaji wote wako vizuri kiafya,
kifikra na morali ni ya hali ya juu kuelekea kwenye mchezo huo dhidi ya
Mapharao.
0 COMMENTS:
Post a Comment