![]() |
| EMIRY (MBELE), SIMBA IKO KATIKA HATUA ZA MWISHO KUMSAJILI. |
Kamati
ya Usajili ya Simba iko katika hatua ya mwisho kumsajili beki wa pembeni,
Nimubona Emiry ambaye ni kiboko.
Emiry ana uwezo wa kucheza kwa ustadi mkubwa beki zote mbili za kulia na kushoto ambazo Simba zaidi wanawategemea Ramadhani Kessy na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.
Emiry raia wa Burundi bado yuko Vital’O ya Burundi na tayari Simba imeanza mazungumzo naye ambayo
yamefika katika nzuri.
Iwapo
watakubaliana, kiongozi mmoja wa Simba anaweza kukwea pipa na kwenda kumsajili
beki huyo anayeaminika ataleta upinzani mkubwa kwa mabeki wa pembeni wa Simba.








0 COMMENTS:
Post a Comment