Mambo yakienda vizuri, Azam TV itakuwa kituo cha kwanza cha
runinga nchini kurusha ‘live’ mechi za Ligi Kuu England kwa Lugha ya Kiswahili.
Hadi sasa uongozi wa Azam TV upo kwenye mipango ya kuhakikisha unarusha
ligi hiyo live kutoka England katika msimu ujao unaotarajiwa kuanza mapema
mwezi ujao.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Tido Mhando, alisema wamejipanga
kuhakikisha wanalikamilisha hilo mapema.
“Tunafanya juhudi kubwa ili
tulifanikishe hilo mapema, ila wahusika ndiyo wenye uamuzi wa mwisho katika
kutupa haki ya matangazo hayo, tumedhamiria pia kuonyesha Ligi ya Hispania.
“Wakati tukipanga haya, tuna nia ya kuboresha muonekano wa ligi
yetu ya Tanzania (Ligi Kuu Bara) msimu ujao ambapo tunataka ionekane katika
ubora wa hali ya juu zaidi,” alisema Tido.
Katika hatua nyingine, Tido alisema katika kipindi hiki cha
kuelekea uchaguzi hadi utakapofanyika, watakuwa wakiwaletea watazamaji wao matangazo
ya matukio mengi kuhusu uchaguzi huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment