Kiungo kiraka
mpya wa Yanga, Joseph Zuttah kweli noma, kwani anamudu kucheza kwa ufasaha
nafasi zaidi ya tatu na kuzua hofu kwa baadhi ya nyota wa timu hiyo.
Zuttah raia wa
Ghana ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo, anamudu
kucheza vizuri beki na winga ya kulia, kiungo mkabaji na mshambuliaji namba
kumi.
Katika mazoezi ya
Yanga yanayoendelea kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar, Zuttah ameonekana
kumudu kucheza vizuri nafasi hizo ambazo zinachezwa na wachezaji nyota wa timu
hiyo.
Juma Abdul anacheza
beki ya kulia, Simon Msuva (winga ya kulia) na Mbuyu Twite na Salum Telela,
sasa wote kwa pamoja mmoja wao anaweza kupoteza nafasi kumpisha Zuttah acheze.
Akimzungumzia Zuttah,
Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm ambaye ndiye aliyeunganisha dili la kuja
kwake nchini, alisema: “Zuttah ni mchezaji mwenye uwezo wa kucheza nafasi nne
ndani ya uwanja na ndiyo maana kila nafasi ninayompanga anacheza vizuri.
“Nilishawahi
kusema kuwa Zuttah ana uwezo wa kucheza namba mbili, sita, saba na kumi, sasa
hapa Yanga nitampanga popote kutegemea na aina ya mechi tutakayokutana nayo.”
0 COMMENTS:
Post a Comment