Azam
FC imeanza michuano ya Kagame kwa kuichapa timu ngumu ya KCC kwa bao 1-0.
Shujaa
wa Azam FC leo ni nahodha wake, John Bocco aliyefunga bao hilo pekee kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Licha
ya ushindi huo, Azam FC walilazimika kufanya kazi ya ziada kutokana na uimara
wa kikosi cha Waganda hao.
Hata
hivyo Shomari Kapombe, Kipre Tchetche, Bocco na Frank Domayo walionekana
kuwasumbua zaidi Waganda hao.







0 COMMENTS:
Post a Comment