Dk Ahmed Twaha ameibuka kuwa mwenyekiti mpya wa klabu
kongwe ya Coastal Union ya Tanga.
Dk Twaha ameibuka na ushindi wa kishindo na kummwaga
aliyewahiI kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi na Makamu Mwenyekiti wa
Coastal Union, Steven Mguto.
Katika uchaguzi huo uliofanyika leo mjini Tanga, Mguto
aliambulia kura 11 kati ya kura 205.
Mguto alikuwa akichuana na Dr Ahmed Twaha katika
kinyang’anyiro cha kiti cha uenyekiti, ambapo Twaha alijizolea jumla ya kura
192 na kutangazwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Alloyce Komba.
Katika nafasi ya makamu mwenyekiti iliyokuwa na mgombea
mmoja, Salum Fakhi alijizolea jumla ya kura 193 za ndiyo, hata hivyo kwa upande
wa Mguto ambaye hakushiriki katika kupiga kura, amepinga matokeo hayo na kudai
kuwa hayakuwa ya haki na kusema kuwa atasonga mbele kudai haki yake ya msingi.
“Siwezi kusema nitafanya nini lakini uchaguzi haukuwa wa
haki na ndiyo maana hata mimi sikupiga kura, kwa sasa bado nina hasira na
kawaida hutakiwi kufanya maamuzi ukiwa na hasira, nitajua nini cha kufanya,
niache kwanza kwa sasa nipumzike,” alisema Mguto.
0 COMMENTS:
Post a Comment