August 20, 2020

 

UONGOZI wa Tanzania Prisons umesema kuwa sababu kubwa ya kuhamishia makazi yao mkoani  Rukwa ni kupisha ukarabati wa hostel zao pamoja na uwanja wao wa mazoezi uliopo Mbeya.


Prisons inayonolewa na Kocha Mkuu,  Salum Mayanga ambaye alikuwa akiinoa Ruvu Shooting msimu wa 2019/20 itatumia Uwanja wa Nelson Mandela msimu huu wa 2020/21 kwa mechi zake zote.


Katibu wa Prisons, Ajabu Kifukwe amesema kuwa msimu wote watakuwa Rukwa na Uwanja wa Nelson Mandela ndio utakuwa Uwanja wa nyumbani.


"Tumeamua kuhamia Rukwa ili kupisha ukarabati wa hostel zetu pamoja na ukarabati wa uwanja wetu wa mazoezi," amesema. 


Mchezo wao wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara Septemba 6 itakuwa dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic