Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu leo
amezindua michuano ya Airtel Rising Star kwa mkoa wa Dare salaam, ambapo timu
kutoka wiliya za Ilala, Temeke na Kinondoni zinashikriki michuano hiyo.
Akifungua michuano hiyo, Zungu
amewatka vijana kutumia vizuri nafasi hiyo ya michuano ya Airtel Rising
kuonekana, kwani kutawapelekea kupata nafasi ya kucheza katika timu kubwa na
kuweza kuendesha maisha yao kwa kupitia mpira wa miguu.
Michuano ya Airtel Rising Stars
imekua ikifanyika kila mwaka nchini kwa lengo la kusaka na kuibuka vipaji vya
wachezaji wenye umri chini ya miaka 17, ambapo wachezaji wenye vipaji
huchaguliwa na kupelekwa katika vituo vya kufundisha soka na wengine
huchaguliwa katika kikosi cha Taifa cha Vijana (Serengeti U17).
0 COMMENTS:
Post a Comment