GARI LA TAMBWE.... |
Straika wa Yanga, Mrundi,
Amissi Tambwe, juzi Jumatano alipata ajali baada ya gari lake aina ya Toyota
Mark X kugongwa na Bajaj katika eneo la Tandale kwa Mtogole wakati akielekea
mazoezini.
Tambwe ambaye ni mfungaji
bora wa msimu wa 2013-2014, amesema ajali hiyo ilitokea baada ya dereva wa
Bajaj kutaka kulazimisha kupita sehemu ambayo hakutakiwa kupita kwa mujibu wa
sheria za barabarani.
“Nilimsamehe palepale kwa sababu sehemu
iliyoharibika haikuwa kubwa ila kama angevunja taa tungekamatana ila
nitaipeleka gereji kwa ajiili ya matengenezo na ipakwe rangi ili iwe na
muonekano wa awali,” alisema Tambwe.
0 COMMENTS:
Post a Comment