Wakati ikiendelea kujifua kwa ajili ya msimu ujao
katika kambi yao iliyopo ndani ya mgodi wa Mwadui, Mwadui FC imedaiwa kuwa ina
mpango wa kwenda Afrika Kusini ‘Sauz’ kujiandaa zaidi.
Katibu wa klabu hiyo, Ramadhan Kilao, amsema, mpango huo upo ikiwa na maana kuwa watakwenda katika nchi
hiyo ambapo ndipo alipo kiungo wa Simba, Jonas Mkude ambaye yupo kwenye
majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika timu ya Bidvest Wits inayoshiriki
Ligi Kuu ya Sauz.
“Tunafanya maandalizi yetu hapa kwa sasa lakini
mpango mzima mambo yakiwa sawa muda wowote tunatarajia kwenda Sauz, wachezaji
wote wapo tayari isipokuwa mmoja tu ndiyo kafiwa na mama yake,” alisema
kiongozi huyo ambaye timu yake inanolewa na Kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
Ikiwa itakuwa hivyo, Mwadui itakuwa imeonyesha
umwamba kwa timu iliyopanda daraja kwenda mpaka Sauz kwa ajili ya kujiandaa na
msimu, jambo ambalo ni nadra kutokea kwenye soka la Tanzania.
0 COMMENTS:
Post a Comment