Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Geofrey Mwashiuya,
ameonekana kuendelea kuandamwa na majanga muda mfupi baada ya kuanza kuitumikia
Yanga.
Ikiwa ni siku chache tangu kuripotiwa kuwa klabu
yake ya zamani ya Kimondo ya Mbeya ipo tayari kupinga yeye kucheza Yanga,
kiungo huyo amepata majeraha ya goti ambayo yatamweka nje kwa siku kadhaa.
Mwashiuya ambaye ameonyesha uwezo wa juu katika
muda huo mfupi aliokuwa klabuni hapo, alipatwa na balaa hilo baada ya kugongana
na beki wa kushoto wa kikosi hicho, Edward Charles.
Daktari wa Yanga, Juma Sufian, amesema kiungo
huyo wa pembeni atakuwa nje ya uwanja kwa siku kadhaa akiuguza mguu wake huo.
“Mwashiuya leo (jana) ameshindwa kufanya mazoezi
na wenzake kutokana na kuumia goti jana (juzi) mazoezini na sasa anaendelea na
tiba.
“Ni matumaini yetu kuwa, baada ya siku tatu
anaweza kurejea uwanjani kuendelea na mazoezi kwa sababu maendeleo yake siyo
mabaya sana,” alisema Sufian.
0 COMMENTS:
Post a Comment