Kikosi cha Mbeya City kinatarajiwa kuanza kujiwinda rasmi kwa
ajili ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara na kimepanga kutumia siku 32.
Ligi inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 22, mwaka huu katika
viwanja tofauti hapa nchini.
Msimu uliopita, Mbeya City ilifanikiwa kumaliza nafasi ya nne licha
ya kuanza ligi kwa kusuasua chini ya
kocha wake mkuu Juma Mwambusi na imefanikiwa kusajili wachezaji watatu huku wachezaji kumi wakiondoka.
Katibu wa timu hiyo,
Emmanuel Kimbe, alisema wanatarajia kuanza maandalizi yao na wataingia kambini
Julai 20, mwaka huu.
“Wachezaji
wanatarajiwa kuingia kambini na
kujiwinda mapema Julai 20, mwaka huu na lengo ni kuhakikisha tunafanya vizuri
na huku ndiko mwalimu ataweza kuainisha mipango yake na hata kuweza kuangalia
michezo ya kirafiki ili kujiweka imara zaidi.
“Kwa sasa hivi tumesajili wachezaji watatu, kama kutakuwa na uhitaji mwingine, tutaweza
kuongeza wachezaji ingawa kila nafasi
sasa hivi ipo vizuri,” alisema Kimbe.
0 COMMENTS:
Post a Comment