July 8, 2015

SSERUNKUMA
Kiungo wa Simba, Mganda, Simon Ssrerunkuma ni kama amefurahishwa na kitendo cha Simba kuachana na Goran Kopunovic ambaye alionekana kuwa mbaya wake kwa kumpiga benchi muda mrefu msimu uliopita na kusema msimu ujao ni  muda wake kuonyesha maajabu.

Nyota huyo wa zamani wa Express ya Uganda, alisema anaamini ujio wa kocha mpya ni chachu pekee kwake kupigana kuhakikisha anapata namba.

Nafasi ya Kopunovic imechukuliwa na Dylan Kerr, raia wa Uingereza ambaye tayari ameingia mzigoni kukiandaa kikosi kuelekea msimu ujao.

Simon amesema: “Nimekuja kivingine, nimejiandaa vema msimu huu na tayari nimesahau yote niliyopitia. Kwa kuwa tuna kocha mpya, naamini uwezekano wa kufanya vyema msimu ujao upo na ndiyo malengo yangu niliyojiwekea,” alisema nyota huyo.


Msimu uliopita, ilifikia hatua Simon akaomba kuachwa kutokana na kushindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza mara kwa mara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic