Uongozi wa Kimondo umepanga kumfikisha Mkuu wa Kitengo cha Habari cha
Yanga, Jerry Muro kwenye ‘kizimba’ cha Kamati ya Maadili na Hadhi za Wachezaji
ya TFF.
Uamuzi wa uongozi huo unatokana na madai kuwa Muro alimdhalilisha
kiongozi wao.
Habari kutoka ndani ya Kimondo zimeeleza wamechukua uamuzi huo baada ya
Yanga kumaliza na klabu hiyo kuhusiana na suala la usajili wa mchezaji Geofrey
Mwashiuya.
“Ni kweli hatua zinachukuliwa, lakini tumeona suala hilo liende
chinchini.
“Muro alimdhalilsiha sana bosi wetu, alizungumza maneno ambayo
yalionyesha chuki na dharau. Huenda anadharau kwa kuwa tuko Mbozi.
“Hajui anaowadharau ni akina nani, hivyo tupe muda tukishawasilisha
madai au mashitaka yetu, halafu tutazungumza rasmi,” kilieleza chanzo.
Juhudi zinafanyika kumpata Muro ili aweze kulizungumzia suala hilo
ambalo linaonekana kubaki binafsi dhidi yake baada ya Yanga kumalizana na
Kimondo, kivyao.
0 COMMENTS:
Post a Comment