Kocha wa makipa wa
Simba, Iddi Salim ameanza kazi yake mjini Zanzibar akiwafua makipa wa kikosi
hicho.
Iddi amekuwa gumzo
kutokana na mazoezi anayoyatoa kwenye Uwanja wa Amaan.
Raia huyo wa Kenya
ameungana na Simba akitokea AFC Leopards, lakini kabla amewahi kuzinoa Gor
Mahia na Harambee Stars.
Pamoja na mazoezi,
kocha huyo amekuwa na vifaa tofauti ambavyo vimeonyesha tofauti kubwa na
mazoezi ambayo wamekuwa wakifanya Simba msimu uliopita.
0 COMMENTS:
Post a Comment