ABAJALO FC YA SINZA, DAR ES SALAAM |
Kwa kuzingatia marekebisho ya Kanuni ya
Ligi Daraja la Pili (SDL) yaliyofanywa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) hivi karibuni, SDL kwa msimu wa 2015/2016
itachezwa katika makundi manne ya timu sita sita kwa mtindo wa nyumbani na
ugenini.
Timu itakayoongoza kundi itacheza Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2016/2017 wakati ya mwisho katika kila kundi
itarudi kucheza Ligi ya Mkoa wake kwa msimu wa 2016/2017.
Makundi ya SDL ni kama ifuatavyo; Kundi
A ni Abajalo FC (Tabora), Singida United (Singida), Mvuvuma FC (Kigoma),
Milambo FC (Tabora), Green Warriors (Dar es Salaam) na Transit Camp (Dar es
Salaam).
Timu zinazounda kundi B ni Bulyanhulu FC
(Shinyanga), JKT Rwamkoma (Mara), Pamba FC (Mwanza), AFC Arusha, Madini FC (Arusha)
na Alliance Schools (Mwanza).
Kundi C ni Kariakoo (Lindi), Mshikamano
FC (Dar es Salaam), Cosmopolitan (Dar es Salaam), Abajalo FC (Dar es Salaam),
Changanyikeni Rangers (Dar es Salaam) na Villa Squad (Dar es Salaam).
Nazo African Wanderers (Iringa), Mkamba
Rangers (Morogoro), Town Small Boys (Ruvuma), Wenda FC (Mbeya), Coca-Cola
Kwanza FC (Mbeya) na Sabasaba United (Morogoro) zitakuwa kundi D.
Klabu nyingi bado hazijatuma jina la
uwanja wa nyumbani, hivyo zinakumbushwa kufanya hivyo haraka ili kurahisisha
upangaji wa ratiba.
Ligi Daraja la Pili (SDL) msimu wa
2015/2016 inatarajia kuanza Oktoba 17 mwaka huu.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA
MIGUU TANZANIA (TFF)
0 COMMENTS:
Post a Comment