Shabiki mkubwa wa Yanga, Ally Yanga
leo nusura azimie baada ya wachezaji wawili wa kikosi chake kukosa penalti.
Amissi Tambwe na Simon Msuva, wote
walikosa penalti kwa nyakati tofauti wakati Yanga ikiivaa Telecom ya Djibout.
Mechi hiyo kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar, ilionekana kuwa upande wa Yanga ambayo ilikuwa ikishambulia kwa
kasi.
Tambwe alianza kupoteza penalti,
baadaye ikapata nyingine, Msuva naye akapoteza.
Ally Yanga alionekana kutulia tuli
huku akiwa ametoa macho kama mtu asiyeamini kilichokuwa kinaendelea.
Baadaye alionekana kupata nafuu baada
ya Yanga kufanikiwa kupata mabao mengine na kufikisha matatu huku malimi
Busungu na Geofrey Mwashiuya waking’ara kwa kufunga mabao hayo matatu.
0 COMMENTS:
Post a Comment