Vijana karibu 600 wamjitokeza leo
jijini Dar es Salaam kuwania kucheza katika kikosi cha Simba B.
Kikosi hicho cha wachezaji wenye umri
chini ya miaka 20 wanatakiwa wachezaji 60 tu.
Kocha Yusuf Macho ‘Musso’ amesema
wanatakiwa vijana 60 kama hatua ya kwanza.
“Wamejitokeza kwa wingi, ni jambo
zuri na tunanaendelea na mchujo,” alisema Musso ambaye ni mchezaji wa zamani wa
Simba.
Mchujo huo umefanyika kwenye Uwanja
wa Mwenge Shooting jijini Dar na unatarajia kuendelea kesho.
MUSSO AKITOA MAELEKEZO |
0 COMMENTS:
Post a Comment