July 15, 2015


Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr amesisitiza kwamba kuna mabadiliko makubwa katika kikosi chake.

Kerr amesema angalau anaanza kuona mabadiliko ya ufiti, kasi kwa maana ya nguvu.

"Kambi ya Lushoto iko katika hatua za mwisho lakini kuna mengi tumejifunza na kujua ni nini cha kufanya.

"Naweza kusema ni hatua ya mwanzo lakini imetuonyesha njia na sasa tunaweza kuanza kuangalia mambo mengine ikiwa ni sehemu nzuri ya kujiandaa," alisema Kerr raia wa Uingereza.

Simba imeweka kambi mjini Lushoto ambako imekuwa ikijiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara 2015-16,

Hata hivyo, bado haijapata hata mechi moja ya kirafiki kwa ajili ya kuanza kupima uwezo wa kikosi chake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic