July 28, 2021


IMEELEZWA kuwa nyota wa Simba, Clatous Chama yupo kwenye hesabu za kuwindwa saini yake na timu moja kutoka nchini Morocco.

Ni Far Rabat ambayo kwa sasa inafundishwa na Sven Vandenbroeck, raia wa Ubelgiji ambaye aliibuka huko msimu huu akitokea Klabu ya Simba.

Baada ya kubwaga manyanga ndani ya Simba kocha huyo ambaye alisema kuwa sababu za kifamilia zilimfanya asepe Simba amekuwa akitajwa kuhitaji saini ya Chama kuongeza makali katika kikosi hicho.

Taarifa zimeeleza kuwa moja ya viungo ambao Sven anawatazama kqa ukaribu ni pamoja na Chama kwa kuwa alikuwa anakubali uwezo wake na hata alipokuwa Bongo alikuwa ni chaguo lake la kwanza.

 Msimu wa 2020/21 Sven alipokuwa akiinoa Simba alishuhudia kiungo wake huyo akiibuka kuwa mchezaji bora ambapo alisepa na tuzo hiyo baada ya kufunga mabao mawili na pasi 10 za mabao jambo ambalo lilimfanya awe na rekodi bora kuliko wote kwa msimu uliopita.

Pia kwa msimu huu wa 2020/21 Chama amekuwa bora ambapo ametoa jumla ya pasi 15 na kutupia mabao 8.


6 COMMENTS:

  1. Hamna hela ya kumzuia nyau nyie, jaribuni muone

    ReplyDelete
  2. Hapo ndio unaona utofauti wa wachezaji wa yanga na wale wa simba. Wakati yanga wanahaha congo, south africa, moroco na kwengineko kutafuta wachezaji, somba wachezaji wake wanagombewa na ahly, kaizer na huko morocco.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Halafu wanaropoka Simba inabebwa

      Delete
  3. Hii ndy maana ya ndege wanaofanana huruka pamoja

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic