Siku chache baada
ya Yanga kumwongezea mkataba mshambuliaji wake raia wa Burundi, Amissi Tambwe,
ameibuka na kudai kuwa thamani yake kwa sasa imeongezaka na kuwa miongoni mwa wachezaji
wa bei mbaya katika kikosi hicho.
Jumamosi
iliyopita, Yanga ilimuongezea mshambuliaji huyo mkataba wa mwaka mmoja na nusu
wa kuendelea kubakia klabuni hapo ambapo hivi sasa ataitumikia mpaka mwaka
2017.
Tambwe alisema
kuwa baada ya kupewa mkataba huo, thamani yake imeongezeka na sasa ni mmoja
kati ya wachezaji wa bei mbaya katika kikosi cha timu hiyo.
Awali, wakati
akijiunga na Yanga akitokea Simba, Tambwe alisajiliwa kwa dau la dola 25, 000
na mshahara wa dola 2, 000 kwa mwezi.
“Thamani yangu
kwa sasa imeongezeka ukilinganisha na kipindi kile nilichojiunga na Yanga
nikitokea Simba.
“Dau langu la
usajili limeongezeka lakini pia mshahara nao umepanda, kwa maana hiyo naweza
kusema kuwa thamani yangu imepanda na mimi ni miongoni mwa wachezaji ghali kwa
kipindi hiki katika kikosi cha Yanga,” alisema Tambwe.
Alipoulizwa kuwa
ni kiasi gani alichopewa na Yanga baada ya mkataba huo mpya, alisema: “ Hiyo ni
siri yangu na klabu, hivyo siwezi kusema lolote juu ya hilo.”
Hata hivyo,
habari za kuaminika kutoka ndani ya Yanga ambazo Championi limezipata zinadai
kuwa nyota huyo amelamba dola 30,000 zaidi ya shilingi milioni 60 za usajili na
atakuwa akilipwa mshahara wa dola 3,000 kwa mwezi, sawa na shilingi milioni 6.
“Uamuzi huo wa
kumwongezea Tambwe mkataba pamoja na malipo hayo, ulifikiwa baada ya uongozi
kutambua mchango wake wa msimu uliopita, pia baada ya kusikia kuwa anawindwa na
FC Lupopo ya DR Congo na St George ya Ethiopia,” kilisema chanzo hicho cha
habari.
0 COMMENTS:
Post a Comment