August 17, 2015

MGOPE...

Na Mwandishi Wetu
JE, unajua hakuna ligi bora ya mchezo wa soka kwa kipindi hiki kama ilivyo ile ya Hispania, maarufu kama La Liga?
Huenda mambo mengine utayasema kwa hisia, lakini kama utachukua kipindi cha miaka 10, yaani kuanzia 2000 hadi 2015, La Liga inaonekana ndiyo bora zaidi.


Kitakwimu na hata kwa hesabu, mfano wachezaji bora wa dunia kuanzia mwaka 2000 wanakuwa 15.

Kwa kipindi chote hicho, 10 wametokea Hispania na watano waliobaki wamegawana, England imechukua mara moja kupitia kwa Ronaldo na Italia mara nne.

Huo unaweza kuwa mfano mdogo wa kuonyesha kweli La Liga ni bora zaidi kuliko ligi nyingine maarufu kama vile Premier League ya England, Bundesliga ya Ujerumani na Serie A ya Italia au Ligue 1 ya Ufaransa.

Azam TV, imeamua kuwasogezea Watanzania ligi hiyo na sasa itakuwa ikionyesha michezo yake moja kwa moja, tena kwa uchambuzi wa Kiswahili. Tena katika mwonekano bora zaidi machoni wa High Definition, maarufu kama HD.

Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Azam Media, Mgope Kiwanga, amezungumza na Championi Jumatatu na kueleza namna ambavyo wapenda soka watakuwa na nafasi ya kuona mechi nyingi zaidi za La Liga.

“Kutakuwa na mechi za moja kwa moja, kila Jumamosi tutaonyesha mechi tatu, Jumapili kutakuwa na mechi mbili. Huenda kukawa na mabadiliko kidogo sana.

“Zile mechi zitakazokuwa zinaonyeshwa wakati mmoja, bado baadaye tutatoa nafasi kuonyesha nyingine ambayo haikuonyeshwa. Lakini hapo tutatoa nafasi kubwa zaidi kwa mechi za timu maarufu hasa kama imegongana na timu ambazo si maarufu sana,” anasema Mgope.

“Utaona ambavyo La Liga ilivyofanya vizuri kwa misimu kumi sasa, msimu uliopita unaweza kuwa gumzo zaidi kwa kuwa mabingwa wa Ligi ya Mabingwa, Ligi ya Europa, wote wametokea Hispania. Usisahau kabla ya Barcelona kuwa bingwa wa Ligi ya Mabingwa, wapinzani wao wakubwa kutoka Hispania, Real Madrid ndiyo walikuwa mabingwa,” anasisitiza.

Mgope anasema, kila kabla ya mechi, mapumziko na baada ya mechi, kutakuwa na uchambuzi katika Lugha ya Kiswahili, ili kumfanya mtazamaji kuelewa zaidi kuhusiana na ligi hiyo bora.

Uchambuzi huo utawafanya wapenda soka wengi kujua mambo mengi kuhusiana na ligi hiyo inayotoa mastaa wengi zaidi duniani kuliko nyingine yoyote.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic