August 17, 2015


Mwanachama mmoja wa CCM ameangua kilio baada ya Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kukatwa kwenye kinyang'anyiro cha wanachowania udiwani eneo la Mbagala Kuu jijini Dar es Salaam.


Mwanachama huyo amesema kumekuwa na fitana za makusudi kuondoa jina la Manji licha ya ushindi wake wa kishindo katika kura za maoni.

Alilalama kwamba Manji ameondolewa kwa kisingizio hakuwepo eneo la tukio lakini alitoa taarifa.

"Manji alitoa taarifa kuwa ni mgonjwa, watu wanajua kila kitu lakini wanataka kutuangusha wananchi wa Mbagala Kuu kwa kuwa tunamtaka.

"Kuna mtu anaonekana ndiyo anaongoza vita hiyo, hatujui ni kwa nini na hili jambo hatutakubali," alisema huku akilia kwa uchungu.

Juhudi zinafanyika kumpata Manji ili atoe ufafanuzi kuhusiana na jambo hilo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic