August 17, 2015


Azam FC imeshinda mechi ya tatu mfululizo katika mechi zote tatu ilizocheza mjini Zanzibar baada ya leo kuichapa JKU kwa mabao 2-0.


Katika mechi iliyomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, Azam FC imeshinda kwa mabao hayo mawili, la kwanza likifungwa na John Bocco aliyepewa pasi na Mudathir Yahaya kabla ya Salum Abubakar 'Sure Boy'.

JKU ambao ni washindi wa pili wa Ligi Zanzibar kama ilivyo kwa Azam FC kwa Tanzania Bara, walijitutumua na kuonyesha soka safi, lakini kasi ya wageni wao ilionekana kuwa juu.

Kabla ya mechi hiyo, Azam FC iliwatwanga KMKM ambayo ndiyo timu ngumu zaidi Zanzibar kwa bao 1-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic