Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Haruna Moshi ‘Boban’,
anajaribu tena bahati yake ya kucheza soka la kulipwa, baada ya kutimkia nchini
Oman kufanya majaribio lakini kuna taarifa nyingine inafafanua kuhusu jinsi Mbeya
City ilivyomkosa kiungo huyo dakika za mwisho.
Miaka kadhaa iliyopita, Boban alikuwa akiichezea Gefle IF
inayoshiriki Ligi Kuu ya Sweden lakini alishindwa kuelewana na kocha wale, Perre Olson ambaye baadaye alitaka abaki lakini akashindwa kumshawishi Boban ambaye alirejea nchini na baadaye kujiunga na Coastal Union baada ya kukaa msimu mzia bila kucheza.
Inadaiwa kuwa Boban ameshamaliza wiki sasa tangu atimkie zake
nchini humo kusaka bahati kwa mara nyingine.
Herry Mzozo ambaye ni kocha wa Friends Rangers ya Ligi Daraja la
Kwanza inayommiliki mchezaji huyo, amesema:
“Boban ameondoka, yupo Oman
kwa muda wa wiki sasa. Kuna timu imemuita ambayo itatajwa baada ya kumalizana
kila kitu. Mbeya City walionyesha nia ya kumtaka tangu mwanzo lakini sijui
ilikuwaje baadaye wakawa kimya.
“Sasa walirejea hivi karibuni kuonyesha kuwa wanamhitaji na
wamejikamilisha lakini ikawa wameshachelewa, mipango ya Boban ilikuwa imeshakaa
sawa, kwa hiyo wakawa wamepishana naye lakini pengine wangekuwa na maamuzi
tangu mwanzo, wangeweza kumchukua,” alifafanua Mzozo.
0 COMMENTS:
Post a Comment