August 31, 2015


Na Saleh Ally, Istanbul
Louis Nani amepiga bao mbili wakati timu yake ya Fenerbahce ikishinda kwa bao 2-1 dhidi ya Antalya Sports katika mechi ya Ligi Kuu Uturuki iliyochezwa jijini hapa.


Antalya Sports anaichezea Samuel Eto’o ambaye ni nahodha na ndiye alitoa pasi ya bao la kusawazisha.
Fenerbahce ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Nani ambayo aliunganisha kwa kichwa krosi safi ya kichwa.

Lakini Antalya wakasawazisha kwa bao lililotokana na pasi mzuri ya Eto’o ambaye alikimbia kwa zaidi ya mita 20 kabla ya kutoa pasi hiyo.
Nani aliukwaa ushujaa wa mechi hiyo mwishoni kabisa ikiwa ni tayari kibao cha kuongeza dakika 6 za nyongeza kikiwa kimeonyeshwa.


Nani alifunga bao hilo kwa mkwaju wa mpira ‘uliokufa’ na kumuacha kipa wa Antalya akiwa hajui la kufanya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic