Kiungo mkongwe, Amri Kiemba
amejiunga na Stand United ya Shinyanga.
Kiemba pamoja na kiungo wa zamani
wa Yanga, Hassan Dilunga wametua Stand United ambayo sasa inadhaminiwa na
kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia.
Msemaji wa Stand United, Deokaji
Makomba amesema wachezaji hao, kila mmoja amesaini mkataba wa mwaka mmoja.
“Kiemba anatarajia kurejea hapa
Shinyanga leo kuungana na wenzake kwa ajili ya kwenda Kahama ambako tutaweka
kambi.
“Pia Dilunga suala lake
limemalizika naye amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Stand, chama la
wana.”
Mara ya mwisho, Kiemba aliichezea
Azam FC ambayo alijiunga nayo akitokea Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment