MARSH WAKATI WA UHAI WAKE AKIWA NA VIJANA WA ACADEMY YAKE. MARSH AMEFARIKI DUNIA MIEZI MICHACHE BAADA YA KUSUMBULIWA KWA MUDA MREFU NA UGONJWA WA KANSA. |
Kipa wa kikosi cha Marsh Academy
amefariki dunia akiwa uwanjani.
Taarifa zilizoifikia SALEHJEMBE,
zimeeleza, Sylvetsre Laang maaurufu kama Chura amefariki dunia baada ya
kukanyagwa akiwa uwanjani.
“Kweli Chura amefariki baada ya
kukanyagwa na fowadi wakati wakiwania mpira. Lakini amefia kwao Mahenge na
taarifa zimeletwa Mwanza,” alieleza Thomas aliyedai ni mmoja wa wahusika wa
Academy iliyokuwa na marehemu Marsh.
“Alikuwa amekwenda kwao Mahenge
kwa mapumziko, huko ndiko matatizo yalipomkuta,” alisisitiza.
TUNAENDELEA KUFUATILIA TAARIFA
ZAIDI KUHUSIANA NA TUKIO HILO.
0 COMMENTS:
Post a Comment