TAMBWE AKIPIGA KICHWA KUFUNGA BAO DHIDI YA PRISONS PICHA: TBC |
Ile mechi ya kirafiki kati ya Yanga na Tanzania Prisons
iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Sokoine, mbali na kutawaliwa na ubabe,
ilisababisha kituko ambacho kilihusisha makocha wa Yanga.
Mechi hiyo ambayo ilitawaliwa na ubabe kwa
wachezaji wa timu zote kucheza kibabe kama vile ni mechi ya ushindani,
ilishuhudia Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm na msaidizi wake, Shadrack
Nsajigwa, wakiingia uwanjani baada ya mchezaji wao kuchezewa faulo.
Wachezaji wa timu zote walionekana kuwa na presha
kubwa kutokana na mchezo huo kuwa wa kasi huku wale wa Prisons wakiwa ndiyo wa
kwanza kuonyesha kuja juu kutokana na kufungwa mabao 2-0.
Kabla ya tukio hilo la makocha hao kuingia
uwanjani, beki wa kushoto wa Yanga, Haji Mwinyi na Zani Kufo wa Prisons walitolewa
nje kwa kadi nyekundu baada ya kuchapana makonde kavukavu.
Katika dakika ya 67, Pluijm na Nsajigwa ambaye
amepewa jukumu hilo kutokana na Charles Mkwasa kuwa bize na Taifa Stars,
walivamia uwanja baada ya kiungo wao, Deus Kaseke kuchezewa rafu na James
Mwasote.
Mara baada ya tukio hilo la rafu, kulitokea
vurugu baina ya pande mbili huku beki wa Yanga, Mbuyu Twite naye akitibuana na
Lambart Sabianka wa Prisons, kuona hivyo ndipo makocha hao wakaingia mpaka
uwanjani wakati mchezo ukiendelea ili kutuliza presha, jambo ambalo
walifanikiwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment