Klabu ya Azam FC, imeeleza masikitiko
yake kutokana na beki Juma Nyosso kumshika makalio nahodha wake, John Bocco kwa
lengo la kumdhalilisha.
Msemaji wa Mbeya City, Jaffar Iddi
amesema wamesikitishwa kwa kiasi kikubwa na kitendo hicho cha Nyosso ambacho
kilinaswa na vyombo mbalimbali ikiwemo blog hii ya SALEHJEMBE.
Nyosso alifanya makusudi
kumdhalilisha Bocco hii ikiwa ni mara ya pili kunaswa na vyombo vya habari
akifanya hivyo.
Msimu uliopita alimfanyia hivyo,
Elius Maguri wakati akiitumikia Simba, akanaswa na blogu hii pamoja na gazeti
namba moja la michezo nchini la CHAMPIONI.
“Vitendo kama hivyo kama alivyofanya
Nyosso havikubaliki hata kidogo, tunaalani kwa nguvu zote kabisa.
“Lakini tunavishukuru vyombo vya
habari kuhusiana na hilo, vimekuwa shahidi wa kila kitu. Lakini pia tunaiachia
TFF, tunajua hadi Rais wa TFF, Jamal Malinzi hilo limemfikia.
“Tunaamini hatua kali zitachukulia
kukomesha vitendo kama hivyo visivyo vya kiungwana,” alisema.
Baada ya kubainika alimfanyia hivyo
Maguri, Nyosso ambaye ni beki wa zamani wa Simba, alifungiwa mechi nane.
0 COMMENTS:
Post a Comment