MANARA AKIMILIKI MPIRA... |
Msemaji wa Simba, Haji Manara
amealikwa kesho kwenda kwenye makao makuu ya klabu ya Yanga, eneo la mitaa ya
Twiga na Jangwani akiwa mtu.
Msemaji wa Yanga, Jerry Muro amesema,
Manara aende Jangwani akiwa mtu kama alivyoahidi kama Simba ingepoteza mechi
yake ya Jumamosi dhidi ya Yanga.
“Kweli ahadi ni deni, alisema atakuja
akiwa mtupu kama Simba ingefungwa na Yanga. Sisi pia tungependa kumualika aje.
‘Napenda kumwambia Manara kwamba
tumeishafanya usafi vizuri kabisa. Hivyo, akipenda anaweza kuja mapema kabisa
ili kutimiza ahadi yake aliyokuwa ameitoa,” alisema Muro.
Simba ilipoteza kwa kufungwa mabao
2-0 dhidi ya Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam, Jumamosi.
Sasa Yanga inaongoza Ligi Kuu Bara
ikiwa na pointi 12 sawa na Mtibwa Sugar na Azam FC, lakini zinatofautiana kwa
mabao ya kufunga na kufungwa.
Lakini Manara alipoulizwa kuhusiana
na hilo, alionyesha kushangazwa na kilichozungumzwa na Muro.
“Sijawahi hata siku moja kutoa ahadi
hiyo, mara zote nimekuwa nikisistiza Simba itashinda na hilo ni jukumu langu
kama kiongozi.
“Suala la kusema nitaenda nikiwa
mtupu sijawahi kusema, pia nashangaa wakati ule Muro alisema atajiuzulu kama
Yanga itafungwa na Simba. Tukawafunga lakini hakuna hata aliyemuuliza,” alisema
Manara.
0 COMMENTS:
Post a Comment