Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles
Boniface Mkwasa amefiwa na mama mkwe.
Mkwasa ameondoka jijini Dar es Salaam
kwenda Iringa ambako atashiriki mazishi.
Kocha huyo ambaye ni mchezaji wa
zamani wa Yanga, mkewe ni mwandishi mkongwe nchini, Betty Mkwasa.
Akizungumza na SALEHJEMBE, Mkwasa
alisema wamepata msiba huo.
“Kweli na mazishi ni Iringa,
nimeondoka Dar es Salaam, tunatarajia kuzika ndani ya siku hizi mbili halafu
nitaungana na wenzangu Morogoro,” alisema Mkwasa.
Mkwasa pia ni Kocha Mkuu wa Taifa
Srars, tayari ameiongoza mechi mbili ambazo zote imetoka sare.
0 COMMENTS:
Post a Comment