September 20, 2015



Bao la John Bocco katika dakika ya 53, limeiwezesha Azam FC kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mwadui FC.


Mwadui FC inayonolewa na kocha mwenye maneno mengi, Jamhuri Kihwelo 'Julio', imeshindwa kutamba ikiwa nyumbani mjini Mwadui.

Licha ya Mwadui kucheza vizuri na kupata penalti iliyoshindwa kuitumia, Azam FC walionekana pia kufanya mashambulizi mengi na kupoteza nafasi.

Kwa ushindi huo, Azam FC nayo imeshinda mechi yake ya tatu mfululizo na kufikisha pointi tisa sawa na Yanga na Simba.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic