Kiungo mwenye kasi wa Manchester United, Memphis Depay
sasa hawezi kusema tena ni urafiki tu kati yake na mrembo Karrueche Tran.
Depay na Karrueche ,27, wameonekana mitaani katika
jiji la Manchester wakifanya manunuzi, huku kukiwa na ‘mtembeo’ unaoashiria
kuficha kitu na si marafiki pekee.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 aliwahi kuonekana
na mpenzi huyo wa zamani wa msanii Cris Brown wa Marekani, lakini ikaelezwa ni ‘marafiki
tu’.
Hata hivyo, baadaye kukawa na taarifa kwamba wana
uhusiano wa kimapenzi. Licha ya kuficha, lakini sasa mambo yanaonyesha kwamba
lazima watakuwa pamoja.
Pamoja na kuonekana mtaani, lakini usiku walionekana
wakiwa katika klabu moja wakila raha.
Mastaa wengi wamekuwa si wepesi kuanika uhusiano
walionao hadi pale unapokolea na hii huonekana wengi kuwa na hifu hadi hapo
mambo watakapokuwa na uhakika nayo, ndiyo huwa tayari kuweka mambo hadharani.
0 COMMENTS:
Post a Comment