Simba
imeendelea na mazoezi yake kwenye Uwanja wa Boko Veterenani jijini Dar es
Salaam huku Kocha Msaidizi, Selemani Matola akisema nguvu wameelekeza kwenye
mechi dhidi ya Stand United Jumatano, wamesahau mambo ya kupoteza dhidi ya
Yanga.
Simba ilipoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, Jumamosi.
“Katika
soka kuna matokeo yanayojulikana, kweli tumepoteza lakini utaona tulicheza
vizuri na kupata nafasi nzuri lakini hatukuzitumia.
“Sasa
tunaachana na ishu ya kupoteza, badala yake tunarekebisha makosa kutokana na
mechi iliyopita baada ya hapo tunaendelea kupambana,” alisema Matola.
Kikosi
hicho chini ya Dylan Kerr na usaidizi wa Matola, kimeendelea na mazoezi kwenye
uwanja huo huo wa Boko Veterani kwa ajili ya mechi hiyo ya kesho ambayo itakuwa
ni ya tano kwa Simba, msimu huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment