Na Saleh Ally
Simba imeshinda mabao 3-0 dhidi ya Kagera, yote yakiwa
yamefungwa na Mganda Hamis Kiiza.
Kiiza ndiye mchezaji wa kwanza kufunga Hat Trick msimu huu.
Utaona sasa gumzo amekuwa ni mshambuliaji huyo ambaye Yanga ilimuacha.
Yanga iliachana na Kiiza, akaonekana hafai. Simba ikaachana na
Amissi Tambwe akionekana hafai, Yanga nayo ikamchukua, sasa anafanya kazi yake
vizuri kama ilivyo kwa Mganda huyo.
Huenda hapa kuna jambo la kujifunza kwa kila upande, yaani Simba
na Yanga na ikiwezekana wanapaswa kuepuka papara katika mambo yao au wahusika
wengi wanaohusika na usajili kuongeza umakini zaidi.
Hilo si la msingi sana, tuwaachie wenyewe. Nimeamua kuandika
makala haya baada ya kukerwa na Msemaji wa Simba, Haji Manara ambaye hakika
nimekuwa nikiona anaondoka katika misingi ya kazi yake.
Sidhani kama inakuwa ni sahihi msemaji wa timu kuzungumza
ukafikia kumfanyia ulinganisho na shabiki wa kawaida yake.
Manara amekuwa akitumia sana neno, “Sisi si timu ya magazeti”,
ikionekana wazi hajui umuhimu wa vyombo vya habari katika suala la ushirikiano
na klabu au timu yake.
Amekuwa akizungumza huenda katika ‘tone’ ya Kikomandoo zaidi
kuliko nafasi aliyonayo. Sitaki kuamini kama Manara halijui hilo au aliipata
nafasi hiyo ya Simba kwa bahati mbaya.
Najua walimteua kufanya kazi hiyo baada ya aliyekuwepo kabla
yake kuonekana hawezi au ameshindwa na hilo lilikuwa wazi. Lakini bado Manara
hajaweza katika kiwango cha kusema hakuna mwingine zaidi yake.
Nimemsikia akihojiwa na E Sport ya Redio ya EFM. Wakati
akiulizwa maswali kuhusiana na maandalizi na suala la mechi yao dhidi ya Yanga,
alianza kueleza kwamba Simba imesajili vizuri sana na kuliko Yanga.
Lakini akaendelea kusisitiza kwamba wao hawakusajili kwa
magazeti, wazo si timu ya magazeti kama wenzao Yanga.
Kauli hiyo, wengi wanaweza kuichukulia kawaida. Lakini ni ile
isiyo sahihi kuzungumzwa na kiongozi au msemaji wa klabu kama Simba.
Manara pia anapaswa kuizungumza hiyo kauli akiwa anaangalia
anazungumzia sehemu gani. Mtaani kwake, au kwenye kilinge, mfano kwenye kilinge
cha kahawa, baa au kwingineko, haiwezi kuwa na tatizo lolote.
Lakini si sehemu ambayo inaaminika yuko kazini, Watanzania
wapenda michezo wakimsikiliza, tena akijibu tofauti na alivyoulizwa.
Anaweza kusema ni utani wao na Yanga, sawa, yuko sahihi. Lakini Manara
au Simba hawana utani na magazeti.
Zaidi ananishangaza kwamba kila kunapokuwa na jambo wanataka
kulitangaza, kawaida huwaalika wana habari na wanaoipa ushirikiano Simba, wengi
zaidi ni wanaotoka kwenye magazeti na kufuatiwa na wale wanaotokea kwenye redio
halafu runinga, mitandao na kadhalika.
Najua viongozi wa juu wa Simba, kamwe hawawezi kumtuma Manara
kuzungumza redioni madudu kama hayo. Kamwe sisemi umefikia wakati wa kumsaidia
au kumuongoza nini cha kuzungumza na wakati gani. Yeye ni mtu mzima, anajua
nini la kufanya kwa kuwa wakati mwingine atazidi kuumega uhusiano mzuri wa
Simba na wanahabari.
Wakati wanazindua jezi, wakati wanatangaza mkataba na kampuni
fulani hivi, wakati wana mechi za kirafiki wakihitaji watu wengi ili kurudisha
gharama na kupata faida, walikuwa wakitaka urafiki na msaada kutoka kwa wana
habari na magazeti yakiwepo.
Kuyadharau kwa kuwa Simba imeshinda mechi tatu mfululizo,
sidhani kama ni sahihi. Simba ikipoteza, ndiyo dharau itaisha, au...
Najua Manara kaishabikia Simba miaka nenda rudi, lakini hakuwepo kwenye matatizo mengi ya Simba ambayo wanahabari wa magazeti walishirikiana kuanzia uongozi wa miaka 20 au 10 iliyopita. Manara kama kiongozi, hana hata mwaka, maana yake hakuwa msaada wakati magazeti yakiipigania Simba inayopaswa kuwa na maendeleo au mafanikio kama ambavyo yanaanza kujitokeza leo taratibu.
Sasa dharau inatokea wapi, kuanza kuonyesha magazeti yanaunga mkono timu fulani na nyingine la. Hivyo anapaswa kuonyesha nidhamu au thamani ya wanahabari. Ajabu wana habari, wanaona sahihi kudharau wana habari wenzao!
Najua Manara kaishabikia Simba miaka nenda rudi, lakini hakuwepo kwenye matatizo mengi ya Simba ambayo wanahabari wa magazeti walishirikiana kuanzia uongozi wa miaka 20 au 10 iliyopita. Manara kama kiongozi, hana hata mwaka, maana yake hakuwa msaada wakati magazeti yakiipigania Simba inayopaswa kuwa na maendeleo au mafanikio kama ambavyo yanaanza kujitokeza leo taratibu.
Sasa dharau inatokea wapi, kuanza kuonyesha magazeti yanaunga mkono timu fulani na nyingine la. Hivyo anapaswa kuonyesha nidhamu au thamani ya wanahabari. Ajabu wana habari, wanaona sahihi kudharau wana habari wenzao!
Anapotaniana na Yanga, basi afanye hivyo. Akumbuke hata mabosi
wake walio madarakani leo, walisaidiwa kwenye kampeni na magazeti pia kwa kuwa
yaliwapa nafasi ya kuzungumza na kuwafikia wanachama wao waliokuwa wapiga kura.
Walioharibu wakiwa ndani ya Simba na kuifanya iwe na mwendo wa
kubahatisha hadi leo, pia walikemewa na magazeti hadi Wanasimba wakaamua
kufanya mabadiliko. Ndiyo Simba ya sasa ambayo imempa ajira Manara na anaitumikia sasa.
Magazeti yanaongozwa na watu, kuyadharau ni kuwadharau wao pia. Itafikia
siku nayo yatamdharau Manara na wanaoumuunga mkono.
Katika hali ya kawaida, kumheshimu anayekudharau ni kujidharau
pia. Kuna sababu ya Manara kubadilisha njia anayoanza kupita, kuamini kama
tayari Simba ni bingwa na anaweza kusema lolote, mbele ya yeyote ni kupotoka, kutojitambua na kudharau wanaomheshimu pia. Nafikiri kazi
hiyo awaachie ma-MC wa kwenye harusi, naye afanye kazi yake kwa weledi,
akiheshimu kazi za wenzake pia.







This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteSalehe nadhani hujui propaganda za Simba na Yanga na nafikiri una lako jambo mathalani yawezekana nawe ni mlengo wa kushoto mwa Manara. Anayo haki na wajibu wa kusema chochote juu ya vyombo vya habari vinavyotoa taarifa kwa udaku hasa kwa suala linalofanywa na Yanga. Nimeona vyombo habari kadhaa vikiibeza Simba kwa usajili uliofanywa. Mfano chombo cha habari fulani siku moja kabla ya kuazna ligi kuu kilisema.. nanukuu "......simba itakutana na Yanga ikiwa na pointi 2 au tatu kulingana na nionavyo mwenendo wake..." mwisho wa kunukuu. Kwa kauli kama hii inaonesha wazi kuwa mwandishi huyo hajui mpira ni nini na hajui matokeo ya mpira yapo uwanjani. Ni haki ya Haji Manara kusema kile anachofikilia kama binadamu.
ReplyDeleteWewe mtoa comment at 8:00AM nadhani bado hujamuelewa Saleh alichokizungumza.Mimi na Saleh wote ni wanachama watiifu na waaminifu wa Simba hilo halina ubishi.Inapofikia kueleza ukweli Saleh anatumia kalamu yake kuhabarisha jamii na hapo hapendelei simba wa watani wetu Yanga.
DeleteManeno ya Haji ni hatari kwa mustakabali wa soka la Tz kwani ni sawa na ile kauli ya Muro eti ukuta wa T/stars ni Yanga ndio maana nigeria hawakupata bao.Hizo ni kauli za kuwagawa waTZ na tayari saleh alishazikemea hapahapa blogini,labda wewe mwenzetu ulikuwa ktk kampeni za kisiasa ndio maana hukuiona hiyo thread!.
Tumfundishe Haji jinsi ya kuongea na wanahabari kwani naye ni binaadam uhenda anateleza sasa tukimwacha ataanguka na kuvunjika mbavu.
Big up sana kaka yangu Saleh Ally kwa kuelimisha vilaza wa tasnia ya habari Tanzania.