Kazi imeanza. Hatimaye, Simba imepata ‘sumu’ hatari ya kuiteketeza
Yanga katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa wikiendi ijayo kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar.
Simba imeipata sumu hiyo baada ya juzi Jumamosi kukaa kikao kizito
kwa saa nne kilichoitishwa na wakuu wa matawi yote ya timu hiyo kujadili na
kutafakari jinsi ya kumfunga mpinzani wao huyo, huku mwenyekiti wa zamani wa
timu hiyo, Hassan Dalali naye akishiriki kikao hicho.
Msimu uliopita katika michezo yote miwili ya ligi, Simba
ilifanikiwa kuvuna pointi nne baada ya kutoka suluhu mchezo wa kwanza, kisha
kuifunga bao 1-0 katika mchezo wa pili.
Mwenyekiti wa Tawi la Mpira Pesa ambao ndiyo walikuwa waandaaji wa
mkutano huo, Ostadh Masoud, alisema kuwa walilazimika kuitisha kikao hicho cha
dharura haraka ili kujadili mapema jinsi ya kuifunga Yanga.
Alisema kuwa katika kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa
Annex Lango la Jiji na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Simba akiwemo
mwenyekiti wa zamani Dalili, walikubaliana kuwa kwa sasa kila mwanachama aifikiria
kwa makini mechi hiyo pamoja.
Aliongeza kuwa mara baada ya kikao kumalizika, kila mmoja aliondoka
na jambo moja tu la mshikamano, nguvu, umoja na kuahidi kuwa watapambana kadiri
wawezavyo ili kuifanikisha timu yao ipate ushindi.
“Tulichokijadili ni jinsi gani tutaweza kumpiga Yanga kama
ilivyokuwa msimu uliopita na tukakubaliana kuwa katika kipindi hiki tuwe na
mshikamano, umoja, tujenge nguvu moja kwa kushirikiana kuiangamiza Yanga.







0 COMMENTS:
Post a Comment