Kiungo wa kimataifa wa Simba, Mzimbabwe, Justice Majabvi, amemjia
juu mwamuzi, Israel Nkongo, kwa kumtupia lawama kuwa ndiye aliyekuwa sababu
kubwa kwa wao kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Yanga, wikiendi
iliyopita.
Majabvi alikuwa miongoni mwa wachezaji walioanza katika kikosi cha
kwanza cha Simba kilichocheza na Yanga na kujikuta kikipokea kipigo cha mabao
2-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar.
Majabvi amesema mwamuzi huyo aliwabeba wapinzani wao Yanga kwa asilimia kubwa, jambo ambalo
liliwaondoa kwenye mchezo.
“Kiukweli sisi tulipoteza
mchezo wetu kutokana na refa (Nkongo) kutuondolea umakini wetu baada ya
kuonyesha mapenzi ya wazi kwa wapinzani wetu na kuwabeba bila ya sababu ya
msingi.
“Nasema hayo kutokana na aina ya uchezeshaji wake ambapo alikuwa
anawapa Yanga faulo hata kama siyo faulo na pia alitoa kadi za njano nyingi
kwetu ili kuweza kutuzima na kuturudisha nyuma, naamini kama refa angekuwa ‘fea’
katika mchezo huu, basi Yanga wasingeweza kushinda,” alisema Majabvi ambaye ana
bao moja mpaka sasa.
Huyu Majavi hana akili,kama Simba walipewa kadi za njano nyingi mbona hawakutozwa faini na bodi ya kaburu kama walivyotozwa Yanga/
ReplyDeleteMpira umewashinda sasa mnakimbilia kwa refarii,kachezeni bao ambalo halina refa!
Nadhani simba ni wagonjwa
ReplyDelete