September 9, 2015


Inawezekana baada ya siku chache mashabiki wenye kiu ya kuona sura ya mtoto wa mwanamuziki, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Latifah, ikakatika baada ya msanii huyo na mzazi mwenzake, Zarinah Hassan, kuweka wazi siku maalum watakayomuonyesha mtoto huyo hadharani.


Tangu mtoto huyo azaliwe takribani siku 30 zilizopita, sura yake imekuwa ikifichwa lakini juzi usiku wazazi wake walitoa tamko kupitia kurasa zao za Mtandao wa Kijamii wa Instagram kuwa Septemba 20, mwaka huu rasmi wataonyesha sura ya mtoto huyo baada ya mdhamini kujitokeza kudhamini zoezi hilo.

“Tarehe 20/9/2015, kwa mara ya kwanza sura ya binti yangu @princess_tiffah tutaiweka hadharani… Je ungependa kujua ni kampuni gani imedhamini video na picha yake ya kwanza? Usikae mbali na mimi… inakaribia,” yalikuwa ni sehemu ya maneno aliyoandika msanii huyo kabla ya muda mfupi ujumbe huo pia kuwekwa tena kwenye ‘akaunti’ ya Zari. 

Kama kawaida, baada ya hayo, kuliibuka ‘comments’ nyingi juu ya ujumbe huo kutoka kwa mashabiki ambapo wapo walioponda kuhusiana na hilo lakini watetezi na waliojibu mashambulizi hayo pia walichukua nafasi yao na kumpongeza msanii huyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic