Mambo yanaonyesha kumnyookea
mshambuliaji wa timu ya taifa, Taifa Stars, Thomas Ulimwengu baada ya jina lake
kufika kwenye timu za Ligi Kuu ya Uturuki na sasa maombi maalum yametumwa kwa
ajili ya kumtwaa nyota huyo.
Ulimwengu ambaye wikiendi iliyopita
alikuwa nchini akiitumikia Stars kwenye mechi dhidi ya Nigeria kwa ajili ya
kuwania kufuzu kushiriki Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka
2017 nchini Gabon.
Ulimwengu aliyetua Mazembe mwaka 2011,
katika timu hiyo inayomilikiwa na tajiri Moise Katumbi, amefunguka kuwa
ukiachana na timu kutoka Uturuki kuonyesha kila dalili ya kumhitaji mpaka
kufikia hatua ya kupeleka barua rasmi klabuni hapo, bado pia kuna mawasiliano
yanaendelea kufanyika kuhusu kuhamia timu za Ufaransa na Ubelgiji kama
ilivyokuwa kwa Mtanzania mwingine anayekipiga klabuni hapo, Mbwana Samatta.
“Kila mmoja ana ndoto zake, bado nina
ndoto kubwa za kucheza Ulaya na kujulikana zaidi na ninaamini muda si mrefu
zitatimia, kuna timu kutoka Uturuki imeleta barua kwa uongozi wa Mazembe,
inaeleza kuhusiana na kunihitaji, kwa sasa siwezi kuitaja lakini mambo
yakishakamilika, basi Watanzania wote watajua.
“Zipo dili nyingine pia kutoka Ufaransa
na Ubelgiji ingawa hazijaonyesha hatua kubwa kama ilivyo hiyo ya kutoka
Uturuki, lakini naamini safari hii nitaenda Ulaya na huu ndiyo wakati wangu.
“Sidhani kama klabu yangu inaweza
kunizuia,” alisema Ulimwengu.
0 COMMENTS:
Post a Comment